Makala

VINYWAJI: Jinsi ya kuandaa 'smoothie'

October 8th, 2020 1 min read

Na DIANA MUTHEU

[email protected]

Muda: Dakika 10

Wanywaji: Watu wawili

Vinavyohitajika

Vinavyohitajika ili kutengeneza kinywaji ‘smoothie’. Picha/ Diana Mutheu
  • ndizi 2 zilizoiva vizuri
  • parachichi ½
  • karoti 1
  • maji glasi 1
  • blenda
  • sukari (si lazima)

Jinsi ya kuandaa

Safisha matunda yako kisha uyakate vipandevipande na kuyaweka ndani ya blenda yako.

Ongeza karoti na maji yako ndani ya blenda hiyo kisha usage vizuri mchanganyiko huo hadi ‘smoothie’ yako ilainike.

Mimina ‘smoothie’ yako katika glasi. Burudikeni.