Makala

VINYWAJI: Jinsi ya kutayarisha sharubati ya mananasi

June 23rd, 2020 1 min read

Na MISHI GONGO

Idadi ya wanywaji: 4

Vitu vinavyohitajika

  • nanasi nusu
  • karoti kubwa 3
  • ndimu ya unga robo kijiko
  • sukari nusu kikombe
Vipande vya mananasi na karoti. Picha/ Mishi Gongo

Namna ya kutayarisha

Anza kwa kuosha matunda yako kisha chambua maganda.

Chemsha karoti zako hadi zilainike halafu epua kutoka motoni kisha weka pembeni.

Chukua mashine ya kusaga matinda (blender), katakata matunda yako pamoja na karoti kisha tia ndani ya jagi la kusagia.

Ongeza sukari, ndimu ya unga na iliki ukipenda katika jagi kisha maji vikombe vitatu.

Saga hadi matunda yako yalainike.

Chukua jagi safi chuja mchanganyiko wako ili kutoa ‘machicha’.

Unaweza kuweka katika jokofu ikawa baridi au unaweza kunywa vivyo hivyo.