Makala

VINYWAJI: Jinsi ya kutayarisha sharubati ya tikitimaji

July 24th, 2020 1 min read

Na MISHI GONGO

KINYWAJI hiki ni kizuri wakati wa joto kwani husaidia kukata kiu.

Idadi ya wanywaji: 4

Vitu vinavyohitajika

tikitimaji robo

ukwaju kofi moja

sukari nusu kikombe

Namna ya kutayarisha

Anza kwa kuosha tikitimaji kisha chambua maganda.

Weka ukwaju katika sufuria, ongeza vikombe viwili vya maji kisha chemsha ukwaju hadi utokote. Epua kutoka motoni kisha weka pembeni upoe.

Chukua mashine ya kusaga matunda (blender), katakata tikitimaji vipande vidogovidogo kisha tia ndani ya jagi la kusagia.

Kamua ukwaju wako kisha toa mbegu ubakishe ukwaju mwororo.

Ongez rojo la ukwaju, sukari, harufu na vikombe vitatu vya maji ndani ya mashine ya kusagia matunda.

Saga hadi matunda yalainike.

Unaweza ukaongeza Pep Rose Concentrate kupata harufu uipendayo.

Unaweza kuweka katika jokofu sharubati ikawa baridi au unaweza kunywa jinsi ilivyo hivyo.