Makala

VINYWAJI: Smoothie ya nanasi, ndizi na tangawizi

October 13th, 2020 1 min read

Na MARGARET MAINA

[email protected]

Muda wa kuandaa: Dakika 5

Wanywaji: 2

Vinavyohitajika

• vpande vya mananasi yaliyoiva kiasi vikombe viwili

• mdizi mbivu 2

• kikombe ½ cha mtindi

• kijiko 1 cha tangawizi

• vanilla extract kwa kijiko cha chai

• barafu kikombe ½

• shurubati ya nanasi au maji kikombe nusu

Maelekezo

Menya na katakata matunda.

Twanga tangawizi.

Weka viungo vyote kwenye blenda au mashine ya kusagia chakula.

Saga mpaka vilainike.

Mimina kwenye glasi na ufurahie kinywaji.