Viongozi wa kanisa warudishia mbunge pesa alizochangisha

Viongozi wa kanisa warudishia mbunge pesa alizochangisha

Na WYCLIFFE NYABERI

KANISA Katoliki, Dayosisi ya Kisii, limemrudishia Mbunge wa Dagoretti Kaskazini Simba Arati mchango wake wa Sh 100,000 alioutoa katika kanisa la Nyamagwa, eneobunge la Bobasi, kaunti ya Kisii, Jumapili iliyopita.

Hii ni kutokana na hatua ya mbunge huyo kujaribu kuhutubia waumini waliokuwa kanisani, kinyume na walivyokuwa wameagiza mapadre washereheshaji.

Ibada hiyo ya kulitakasa kanisa jipya la Wakristu wa Nyamagwa ilikuwa ikiongozwa na Mwakilishi wa Papa nchini Kenya na Sudan Kusini, Hubertus Matheus Maria van Megen na ilikuwa ikiendelea vyema.

Lakini kuelekea mwisho wa sherehe, kulizuka utata pale uongozi wa kanisa uliwaruhusu Seneta wa Bungoma, Moses Wetangula na mbunge wa Kiminini, Chris Wamalwa kuhutubia waumini ilhali wanasiasa wa ‘nyumbani’ waliagizwa wangezungumza nje baada ya misa.

Ni mbunge wa eneo hilo tu Bw Innocent Obiri aliyezungumza na kazi yake ilikuwa kuwaalika Mabw Wetangula na Wamalwa.

Padri mmoja ambaye hakutaka jina lake litajwe, alisema uongozi wa kanisa Katoliki Kisii ulifikia uamuzi kumrejeshea Bw Arati pesa zake baada ya majadiliano ya kina.

“Ikiwa wananirudishia pesa mbona warejeshe sehemu ya hela hizo? Nilichanga kiasi kikubwa ikizingatiwa niliwafadhili walionisindikiza huko,” Arati akasema.

You can share this post!

Juventus wajinyanyua ligini na kupepeta limbukeni...

VALENTINE OBARA: Tujihadhari sana Pwani isigeuke kuwa Sodoma

T L