Viongozi wa ODM wataka Obado atimuliwe chamani

Viongozi wa ODM wataka Obado atimuliwe chamani

Na IAN BYRON

VIONGOZI wa Chama cha ODM, tawi la Migori wametaka makao makuu ya chama hicho kuanzisha mpango wa kumtimua Gavana wa Kaunti ya Migori, Okoth Obado, chamani.

Hii ni baada ya gavana huyo kutangaza kuwa anajiunga na Chama cha People’s Democratic Party (PDP).

Katika mkutano uliohudhuriwa na viongozi wa ODM tawi la Migori jana, Katibu na mwenyekiti wa chama cha ODM Mabw Joseph Olala na Phillip Makabong’o walimpa Bw Obado makataa ya siku saba kujiuzulu kutoka kutoka ODM.

“Kufuatia tamko la Bw Obado la kuhama chama cha ODM, anafaa kuacha kiti chake cha ugavana baada ya wiki moja na ashughulikie chama chake kipya cha PDP. Asipojiuzulu kama gavana basi uongozi wa kaunti utapendekeza kuondolewa kwake na afisi yetu ya kitaifa,” Bw Olala alisema.

Uhusiano kati ya Bw Obado na ODM haujakuwa mwema kwa miaka mingi, na wakati huu amejitokeza wazi kupanga kuzima umaarufu wa chama hicho katika Kaunti ya Migori.

 

You can share this post!

Ramadhan kupiga breki siasa moto za kumrithi Joho

Mwanamume amshtaki Magara akidai ni babake