Habari Mseto

Viongozi waapa kuurejesha mlima 'ulionyakuliwa na Criticos'

January 28th, 2019 2 min read

Na LUCY MKANYIKA

VIONGOZI wa Kaunti ya Taita Taveta wameapa kuhakikisha kuwa mlima wa Salaita unaodaiwa kunyakuliwa na aliyekuwa mbunge wa Taveta, Bw Basil Criticos unarudishwa kwa umma. ?

Bw Criticos alizungusha ua la stima katika mlima huo kwa madai kuwa ardhi hiyo ni yake. ? Mlima huo una umaarufu wa kihistoria kwa kuwa vita vya Kwanza vya Dunia kati ya majeshi ya Uingereza na Ujerumani vilipiganiwa hapo.

Gavana Samboja na baadhi wa wawakilishi wa bunge la kaunti walisema kuwa hawatakubali mtu mmoja kumiliki eneo la kihistoria kama hilo. ? Bw Samboja alisema kuwa kufungwa kwa eneo hilo kulitatiza sherehe za kuadhimisha miaka 100 tangu kumalizika kwa vita hivyo.

“Mimi mwenyewe nilishindwa kuhudhuria sherehe hizo kwa kuwa eneo hilo lilikuwa limezungushwa ua la umeme. Hatutakubali hayo,” akasema Bw Samboja.

Alisema visa vya dhuluma za mashamba vimekuwa vikiripotiwa katika eneo hilo tangu jadi.

“Hata kama mtu anapenda ardhi kiasi gani wawezaje kupenda mlima?” akauliza. ? Wakati wa sherehe hizo mwaka jana, baadhi ya wageni mashuhuri waliokuwa wamezuru Salaita walishindwa kukwea mlima huo baada ya Bw Criticos kufunga lango la kuingia katika sehemu hiyo.

Balozi wa Uingereza, Bw Nick Hailey na mwenzake wa Ujerumani, Bi Annette Gunter walikuwa miongoni mwa wageni hao. ? Gavana huyo aliitaka serikali kuingilia kati ili kusuluhisha mzozo huo katika kipande hicho cha ardhi.

“Serikali ina uwezo na maafisa wa polisi ambao wanaweza kung’oa ua hilo,”akasema. ? Alionya kuw serikali ikishindwa, viongozi na wenyeji watachua hatua.

“Sitaki kuongoza wenzangu na wananchi kufanya hiyo kazi kwa kuwa nina imani kuwa serikali kuu itafanya hivyo,”akasema. ? Aidha, Samboja aliapa kuhakikisha kuwa ardhi za umma na wananchi zilizonyakuliwa zinarejeshwa ili kukomesha swala la unyanyasaji.

Alidai kuwa baadhi ya wamiliki wa ardhi wamekuwa wakiwatatiza wenyeji kwa kuzungusha ua sehemu za umma kama vile barabara.

“Hatukatazi mtu kuuza ardhi yake, lakini kwa nini mtu anauza ardhi hadi barabara ya umma?”akasema. ? Aidha, mwakilishi wa Wusi/Kishamba Justine Juma alisema kuwa mlima wa Salaita lazima ulindwe kwa vizazi vijavyo.

“Vizazi vijavyo vitapata historia ya vita hivyo ikiwa mlima huu hautanyakuliwa na mtu binafsi,”akasema. ? Vilevile, mwakilishi wa Mboghonyi Bw Jones Maskuj alisema kuwa baadhi ya mabwenyenye wamenyakua ardhi ya wenyeji na kuwabakisha maskwota. ? Aliitaka serikali kuin