Habari Mseto

Viongozi wagawanyika kuhusu kaunti kubadilishwa jina

May 21st, 2018 1 min read

Na ALEX NJERU

MJADALA kuhusu ikiwa Kaunti ya Tharaka-Nithi inafaa kubadilishwa jina ili iwe Kaunti ya Meru Kusini umezidi kusababisha mgawanyiko kati ya wanasiasa, wanataaluma na Baraza la Wazee wa Njuri Ncheke.

Chama cha Wanataaluma wa Ameru (AMPA) na Baraza la Wazee wa Ameru Njuri Ncheke, wanataka jina hilo libadilishwe lakini wanasiasa wamesisitiza hilo halitafanyika.

Akizungumza jana katika kijiji cha Karwamba, Seneta Kithure Kindiki alimwambia Naibu Chansela wa Chuo Kikuu cha Chuka Erastus Njoka, ambaye amekuwa katika mstari wa mbele kutaka mabadiliko hayo, akomeshe shinikizo zake.

Wanataaluma wamesisitiza hatua hiyo inalenga kuleta umoja wa Wameru wote na wanataka kuwe na kaunti za Meru Kaskazini na Meru Kusini, badala ya Meru na Tharaka-Nithi ilivyo sasa.