Viongozi washinikiza Kuria atimuliwe kwa mpango wake wa GMO

Viongozi washinikiza Kuria atimuliwe kwa mpango wake wa GMO

NA SHABAN MAKOKHA

BAADHI ya viongozi kutoka eneo la Magharibi wanataka wabunge waanzishe hoja ya kutokuwa na imani na Waziri wa Biashara, Moses Kuria.

Gavana wa Kakamega, Fernandes Barasa na naibu wake Ayub Savula walisema kuagizwa kwa mahindi ya GMO kutaathiri uzalishaji wa mahindi ya humu nchini.

Bw Barasa aliongeza kwamba wanaoathirika pakubwa ni wakulima wa Bonde la Ufa na maeneo ya Magharibi.

“Serikali inapaswa kutoa kipaumbele cha kwanza kwa mahindi yanayozalishwa na wakulima wa humu nchini. Wakulima wanahitaji kufikia Bodi ya Kitaifa ya Nafaka na Mazao ili kuuza akiba ya mahindi ambayo yamehifadhiwa majumbani mwao. Wasagaji wanawanyonya kupitia matapeli,” Bw Barasa akasema.

Imeibuka kuwa wakulima wamekataa kuachilia mahindi ya takriban magunia milioni 20 kwa wasagaji kutokana na bei duni.
Bei ya mahindi imefikia rekodi ya Sh5,000 kwa kila gunia la kilo 90 huku kukiwa na uhaba mkubwa nchini.

Wakati wa kampeni kuelekea uchaguzi mkuu wa Agosti 9, uongozi wa Kenya Kwanza uliahidi kufufua sekta ya kilimo.

Rais William Ruto, ambaye alikuwa mgombea urais wa Kenya Kwanza, alikuwa ameahidi kupunguza gharama ya maisha kwa kuongeza uzalishaji wa chakula hasa mahindi.

  • Tags

You can share this post!

KOMBE LA DUNIA FIFA 2022: Ghana walima Korea Kusini na...

Makatibu: Mahakama yatupilia mbali kesi za kupinga bunge...

T L