Michezo

Vipusa wasagaji wa timu ya taifa ya USA kufunga ndoa

March 18th, 2019 1 min read

NA MASHIRIKA

WACHEZAJI wawili wa kikosi cha soka ya wanawake nchini Amerika, Ali Krieger na Ashlyn Harris wamefichua mipango yao ya kufunga pingu za maisha mwishoni mwa mwaka huu.

Wakitumia mitandao ya Twitter na Instagram, wasagaji hao pia walikiri kwamba wamekuwa wakihusiana kimapenzi kwa kipindi cha miaka tisa iliyopita.

Harris, 33, ni kipa wa timu ya taifa ya USA na kikosi cha Orlando Pride nchini Amerika. Alimvisha mwenzake Krieger, 34, pete ya uchumba jijini Florida, Amerika mwaka jana.

Katika mahojiano yake na gazeti la The Sun wiki jana, Harris alikiri kwamba alianza kuvutiwa na Krieger mnamo 2010 wakati majukumu ya kuichezea timu ya taifa yalipowakutanisha kambini.

“Tulianza kuketi pamoja mara kwa mara tuliposafiri kwenye basi au ndege kwa mechi za mbali. Hili na mapenzi lilikuja baadaye kwa kuwa mara nyingi tulikuwa tukizungumzia maazimio yetu ya baadaye maishani na kitaaluma,” akasema Harris.

Wiki ijayo, wawili hao watakuwa wageni katika hoteli mpya inayomilikiwa na nyota wa Barcelona, Lionel Messi kwenye ufuo wa Ibiza nchini Uhispania ambayo itandaa hafla ya ngono itakayowashirikisha wanawake pekee.

Kwa mujibu wa vinara wa The Skirt Club ambao wataendesha hafla hiyo ya siku nne, hoteli ya MiM Ibiza Es Vive (awali ikiitwa Es Vive) iliyonunuliwa na Messi mwishoni mwa mwaka jana, itatoa jukwaa mwafaka kwa wasagaji 9,000 kuponda raha katika vyumba 52 vya mkahawa huo wa kifahari.

MiM Ibiza Es Vive ilipata umaarufu mkubwa miongoni mwa mahawara mwishoni mwaka jana baada ya The Skirt Club kutumia ukumbi wa hoteli hiyo kuendeshea biashara ya huduma za ngono ya haraka kwa wanasoka.