Habari Mseto

Visa vingine 307 vya corona vyaripotiwa

July 1st, 2020 1 min read

ANGELA OKETCH na FAUSTINE NGILA

Kenya imerekodi visa vya maambukizi ya njuu zaidi katika saa 24 zilizopita huku watu 307 wakithibitishwa kuwa na corona kutokana na sampuli 3,591 zilizopimwa , na idadi ya maambukizi ikifika 6,673.

Maambukizi yamezidi kwa sababu watu wengi hawafuatilii maagizo yaliwekwa ili kudhibiti virusi vya corona, Waziri Msaidizi wa Wizara ya Afya Rashid Aman alisema katika hotuba ya kila siku.

Dkt Aman  alisema kwamba maaabukizi zaidi yanaashiria kwamba Kenya inaweza fika kileleni cha maambukizi kati ya Juli na Septemba.

Wakati huo huo Dkt Aman alisema watu wengine 50 waliruhusiwa kwenda nyumbani baaada ya kupona virusi vya corna huku idadi ya waliopona ikifikia 2,089 naidadi ya vifo kufikia 149 huku mtu mmoja akifari usiku.