Kimataifa

Visa viwili vya Ebola vyaripotiwa DRC

August 25th, 2020 1 min read

NA PATRICK ILUNGA

Idara ya kupigana  na ugonjwa  wa Ebola ya  Jamhuri ya Demokrasia ya Congo imethibitisha  visa viwili vya ugonjwa huo eneo la Lotumbe, jimbo la Equateur.

Visa hivyo viliripotiwa Imbonga na Nkasa  huku kifo kimoja kikiripotiwa nje ya kituo cha kutibu  Ebola.

Tangu kuanza kwa janga hilo la Ebola, visa 92 tayari vimethibitishwa.

Vifo 42 tayari vimeripotiwa kwenye janga la 11 la Ebola DRC wakati janga la 10 la ugonjwa huo ambalo liliua watu 2,200 Iturina Kivu Kaskazini  lilithibitishwa kumalizwa Juni iliyopita na serikali.

Maeneo yalioathirika nia pamoja na Bikoro, Bolomba, Iboko, Mbandaka, Lotumbe, Wangata na Ingende.

TAFSIRI NA FAUSTINE NGILA