Visa vya wizi wa mita za maji vyakithiri Malindi

Visa vya wizi wa mita za maji vyakithiri Malindi

NA ALEX KALAMA

IDARA ya maji katika eneobunge la Malindi kaunti ya Kilifi imesema inapoteza shilingi laki sita kila mwezi kutokana na wizi wa mita za maji unaoendelea katika eneo hilo.

Kulingana na mkurugenzi mkuu wa kampuni ya maji ya Mawasco, Gerald Mwambire, visa vya wizi wa mita hizo vimekithiri sana hali inayochangia ukosefu wa maji katika sehemu nyingi za eneo hilo la Malindi.

“Mji wa Malindi umekuwa na wizi wa mita sana hizi mita za chuma,watu wanaendelea kuiba zile mita zile funguo, valve ambazo nyingi ni za brass. Hii imekuwa shida kubwa sana sababu tunaona karibu kila wiki tunapoteza kama mita 100 na mita moja bei ya chini ni Sh6,000. Hizo kwa jumla ni Sh600,000 ambazo tunapoteza kila mwezi,” alisema Bw Mwambire.

Hata hivyo Mwambire amelaumu wafanyibiashara wanaonunua vyuma chakavu huku akiitaka serikali kudhibiti biashara hiyo akisema kuwa imechangia wizi wa mifereji ya maji.

“Mita ikiibwa tunapoteza maji na pia watu wanakosa maji. Hali hii ninaona inasababishwa na wezi wanaopeleka kwa wauzaji wa vyuma chakavu yaani scrap metal. Tunashukuru sana rais wakati uliopita alikuwa amefunga kabisa biashara holela ya aina hii na wizi wa mita ukapungua. Biashara hii ilipofunguliwa tena wizi wa mita ukaanza kupanda tena,” alisema Bw Mwambire.

  • Tags

You can share this post!

Masit adai kushurutishwa afuate nyayo za wenzake na ajiuzulu

Bei ya omena kupanda wavuvi wakitii marufuku

T L