Vishale: Maafande wa Nakuru Mashariki ndio mabingwa wa taji la Healing The Boot

Vishale: Maafande wa Nakuru Mashariki ndio mabingwa wa taji la Healing The Boot

NA JOHN KIMWERE

MAAFANDE wa Kenya Police kutoka kituo Nakuru Mashariki wametazwa mabingwa wa taji la Healing The Boot, kwenye mechi za vishale zilizofanyika kwenye ukumbi wa kituo cha polisi cha Bondeni, Kaunti ya Nakuru.

Shindano hilo la makala ya pili lilishuhudia ushindani mkali baina ya maafande wa Nakuru Mashariki, Nakuru Kaskazini na Njoro.

Maafande wa Nakuru Mashariki chini ya nahodha, Helena Kabukulu walipambana mwanzo mwisho na kubeba taji hilo kwa kusajili alama 20.

Nayo timu ya Nakuru Kaskazini iliibuka ya pili kwa alama 19, mbili mbele ya wenzao wa Njoro. Kuresoi Kaskazini ilimaliza ya nne kwa kuzoa pointi 13, moja mbele ya Gilgil sawa na Subukia.

”Ninapongeza wachezaji wenzangu kwa kujitahidi na kulemea wapinzani wetu,” nahodha wa Nakuru Mashariki alisema na kuongeza kuwa mechi za kipute hicho zilivutia maafande wengi.

Mashindano ya ngarambe hiyo yaliandaliwa na kamanda wa polisi Kaunti ya Nakuru, Beatrice Kiraguri ili kusaidia maafisa wa polisi kuondoa mawazo ya kazi nyingi.

Kamanda huyo anashikilia kuwa wataendelea kuandaa mechi hizo kwa ushirikiano na viongozi wa Chama cha Vishale cha Kenya (KDA) eneo hilo.

  • Tags

You can share this post!

Raila kifua mbele kura ya maoni ya TIFA

Abuni apu ya ‘Mkulima Young’ inayosaidia...

T L