Habari Mseto

Vita vya bunduki vyaacha mmoja amefariki Samburu

October 27th, 2020 1 min read

NA GEOFFREY ONDIEKI 

Mwanamume wa miaka 20 aliuawa na wengine wawili kujeruhiwa kwenye vita vilivyohusisha bunduki eneo la Simale Kaunti ya Samburu.

Polisi walisema kwamba vita hivyo vilizuka Jumatatu baada ya kikundi cha vijana kutofautiana.

Kamanda wa polisi wa Samburu Kaskazini Tom Makori alisema kwamba waliopata majeraha wanatibiwa kwenye hospitali ya Baragoi. Aliongeza kwamba mwili wa aliyefariki ulipelekwa kwenye chumba cha kuhifadhi maiti cha hospitali ya rufaa ya Samburu..

Bw Makori alisema kwamba polisi walitumwamaeneo hayo kuchunguza kilichoendelea kati ya makundi hayo mawili.

“Bado hatujabaini kilochoelekea vita hiyo hila tumetuma polisi eneo hilo kulinda na kuchunguza kilichotokea,”alisema Bw Makori.

Kundi la walinda usalama kutoka Baragoi na Tuum wanalinda eneo hilo lililoathirika ili kuleta amani.

Tafsiri na Faustine Ngila