VITUKO: Harusi tunayo! Staa Rashford avisha Lucia pete ya uchumba

VITUKO: Harusi tunayo! Staa Rashford avisha Lucia pete ya uchumba

IMEKUSANYWA NA CHRIS ADUNGO

MSHAMBULIAJI wa Manchester United, Marcus Rashford, amepiga hatua katika safari ya kuhalilisha uhusiano wake na Lucia Loi, kwa kumvisha kipusa huyo pete ya uchumba.

Rashford, 24, alifanya hivyo Jumanne usiku walipokuwa wakiponda raha katika mkahawa mmoja jijini Los Angeles, Amerika.

“Rashford amekuwa akipanga kumfanya Lucia kuwa wake wa halali kwa muda mrefu. Alifanya kitu spesheli Jumanne mbele ya marafiki wa karibu akiwemo sogora mwenzake ugani Old Trafford, Jesse Lingard. Alimvisha Lucia pete ya almasi iliyogharimu Sh45 milioni,” akasema msemaji wa familia ya fowadi huyo.

Rashford na Lucia, 24, walitua Amerika siku moja baada ya Man-United kukamilisha msimu kwa kichapo cha 1-0 kutoka kwa Crystal Palace, kwenye Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) ugani Selhurst Park, Jumapili.

Wawili hao walirudiana mwanzoni mwa mwaka huu baada ya kutengana kwa miezi minane. Mrembo huyo ni afisa wa uhusiano mwema katika kampuni moja ya sukari nchini Uingereza.

Rashford alianza kumtambalia 2013 wakiwa wanafunzi katika shule ya Mersey eneo la Ashton, jijini Manchester., amekuwa nguzo muhimu katika safari ya kuimarika kwa Rashford kitaaluma.

Alianza kumfungulia Rashford mzinga wake wa asali mnamo 2013 wakiwa wanafunzi katika shule ya Mersey, eneo la Ashton, jijini Manchester.

Baada ya kutengana na dume lake mnamo Mei 2021, Lucia alifuta picha zao zote mitandaoni, jambo ambalo Melanie Maynard ambaye na mama wa Rashford alikiri liliathiri mwanawe kisaikolojia na kuchangia kushuka kwa makali yake kambini mwa Man-United.

“Rashford alikosa utulivu. Aliumia sana kimawazo Lucia alipofunganya virago na kujiendea zake walipokosana mwaka jana. Uhusiano wao ulivurugwa na ‘lockdown’ ambayo iliwaweka katika ulazima wa kuishi pamoja kwa mara ya kwanza kwa zaidi ya miezi 12. Bila shaka walitofautiana kifikra kuhusu mambo fulani,” akaeleza Melanie.

  • Tags

You can share this post!

Nilikuwa mstari wa mbele kuhakikisha Lamu inakuwa na lami...

WANDERI KAMAU: Tusikubali misamaha ‘duni’...

T L