Habari Mseto

Vivo Energy yapunguza bei ya mafuta kwa Sh13

August 17th, 2018 1 min read

Na BERNARDINE MUTANU

KAMPUNI ya Vivo Energy imepunguza bei ya mafuta ya injini ya V-Power, ambayo huuzwa na vituo vya Shell kwa lengo la kuvutia wateja zaidi.

Kampuni hiyo imepunguza bei ya mafuta hayo kwa Sh13. Ni mara ya kwanza kwa kampuni hiyo kupunguza bei ya bidhaa, miaka saba baada ya kuzindua V-Power.

Bei ya bidhaa hiyo huwa haidhibitiwa na Tume ya Kudhibiti Kawi (ERC) kwa sababu mafuta hayo huwa yanaagizwa moja kwa moja kutoka Mashariki ya Kati na Vivo Energy.

Ni kumaanisha tofauti ya bei kati ya Shell V-Power na Shell FuelSave Unleaded ni Sh12 kwa lita moja ikilinganishwa na Sh25 awali.