Viwanda vyafungwa mahindi yakikosekana

Viwanda vyafungwa mahindi yakikosekana

Na BARNABAS BII

WAFANYAKAZI wengi katika baadhi ya viwanda vya usagaji mahindi maeneo ya Magharibi na Kati mwa Kenya wamepoteza ajira kutokana na usitishaji wa shughuli za usagaji unaosababishwa na uhaba mkubwa wa mahindi.

Uhaba wa mahindi umesababisha bei ya unga kupanda huku Wakenya zaidi ya milioni tatu wakikabiliwa na njaa.

Kufikia sasa, angalau viwanda 10 vya kusaga vimewalazimisha wafanyakazi wao waende likizo ya lazima baada ya kufungwa kwa muda kutokana na upungufu mkubwa wa mahindi. Uhaba wa mahindi unahusishwa na kupungua kwa mavuno kwa asilimia 4.3 kutoka magunia milioni 44.0 mwaka 2019 hadi magunia milioni 42.1 msimu uliopita.

“Wasagaji wengi wamekuwa wakivumilia hasara kwa muda wa wiki mbili zilizopita. Hata hivyo, baadhi yao walisitisha shughuli baada ya bei ya mahindi kuuzwa Sh3,200 kwa gunia la kilo 90 na wanangoja kuendeleza shughuli hizo ikiwa watapata hifadhi ya kutosha,” akasema Kipngetich Mutai, mwenyekiti wa Chama cha Wasagaji cha Grain Belt Millers (GBMA).

Kadhalika, alisema kuwa asilimia 80 ya wanachama wao wameondolewa kwenye biashara.

kutokana na kupanda kwa bei ambayo imechangiwa na kuingilia kati mchakato wa usambazaji wa mahindi na makampuni ya biashara za kibinafsi.

Baadhi ya viwanda vilivyoathiriwa sana ni vilivyo katika maeneo ya Bungoma, Busia, Kisumu, Narok, Kajiado na mingine minne ya Kati mwa Kenya.

  • Tags

You can share this post!

Raila atakiwa aandamane na Uhuru ziara ya Mlima Kenya

TUSIJE TUKASAHAU: Rais afaa kutatua tatizo la wakulima wa...

T L