Vurugu zatatiza shughuli ya kujumlisha kura Malindi

Vurugu zatatiza shughuli ya kujumlisha kura Malindi

NA ALEX KALAMA

SHUGHULI ya kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi katika kituo kikuu cha kujumlisha kura cha eneobunge la Malindi imesitishwa baada ya makabiliano makali kuzuka kati ya viongozi wa vyama vya United Democratic Alliance (UDA), Pamoja African Alliance (PAA) na Orange Democratic Movement (ODM) kupigana ndani ya kituo hicho baada ya kutofautiana vikali kuhusu masanduku ya kura.

Hii ni baada ya ajenti wa chama cha UDA Elvis Makanga Tuva kuibua malalamishi kuhusu masanduku sita ya kura aliyodai yalikosa mwenyewe na hayajulikani ni ya nani na yalitoka wapi kuchanganywa na yale ambayo tayari yalikuwa yamehesabiwa.

Hatua ambayo iliyoibua maswali chungu nzima na kupelekea baadhi ya viongozi wa chama cha UDA na chama cha PAA kupinga kuendelea zoezi hilo hadi jambo hilo liweze kutatuliwe,lakini swala hilo lilipingwa vikali na wale wa chama cha ODM na kusababisha kutokea kwa vurugu.

  • Tags

You can share this post!

Ruto afagia upinzani katika ngome yake

KAULI YA WALLAH BIN WALLAH: Kila kitu kinakuja na kupita...

T L