Makala

Vya kuzingatia ili kuondoa kitambi

December 7th, 2020 2 min read

Na MARGARET MAINA

[email protected]

KULA samaki, nyama, mboga za majani aina yote, mayai ya kienyeji na siagi.

Usile au punguza kula vyakula wa sukari na wanga (wali, mkate, chapati, baga yaani burger, mandazi na jamii zingine zitokanazo na ngano, tambi, viazi vitamu na viazi mviringo).

Jitahidi kula pale tu unapokuwa una njaa na sio kwa sababu kuna chakula mbele yako, na hakikisha kila unapokuwa una njaa hakikisha umekula hadi utosheke.

Tafiti zinaonyesha kwamba unapopunguza sukari kwa kupunguza vyakula vya sukari na wanga, Unapunguza kiwango cha insulini kwenye damu kinachofanya kazi ya kuhifadhi nishati katika mfumo wa mafuta na matokeo yake mwili utaanza kuunguza mafuta na kuwa mtu wakutosheka na kushiba haraka na kuondokana na tatizo la ulaji holela.

Ulaji wa nyama

Nyama ina protini na pia ina mafuta. Hivyo kama unahitaji kupunguza uzito, epukana na aina yoyote ya nyama .Epuka kula nyama nyekundu na ule u nyama nyeupe.

Samaki

Unaruhusiwa kula samaki wa aina yoyote kwani samaki wana kiwango kingi sana cha mafuta mazuri ambayo huongeza Omega 3 katika mwili wako ambayo kazi kubwa ni kulainisha mishipa na kufanya mzunguko wa damu ufanye kazi katika ufanisi wa hali ya juu kiafya. Kula sangara, sato, samaki wa baharini n.k.

Mayai

Unatakiwa ujue kuwa mayai ni chanzo kizuri sana cha viini lishe vikuu kama mafuta na protini. Hivyo unaweza kutumia mayai ya kuchemsha au kukaanga na mafuta ya alizeti,mafuta ya mizeituni au ya nazi.

Mboga za majani zinazostawi juu ya ardhi

Mboga za majani zina kiwango kingi sana cha nyuzi (fibers) na hivyo zitakufanya muda wote tumbo lako liwe limeshiba na kiwango cha insulini kuwa katika usawa muda wote. Mbali na hivyo utajipatia madini kama manganese,selenium ambayo vinasaidia shughuli za mwili zifanyike katika kiwango stahiki na mwili kuweza kuunguza mafuta.

Matunda

Usipendelee sana kula matunda kwa sababu matunda yako unapokuwa umekula angalau matano kwa siku ni sawa kama umekunywa soda milimita 500. Hivyo jitahidi kuepuka. Na kama unahitaji kutumia kama juisi hakikisha unatumia blenda ila hakikisha juisi yako umekunywa kati ya dakika 15 kwa sababu baada ya dakika hizo vitamini zitakuwa sio hai tena kwa sababu ya mwanga na joto wakati wa kusaga juisi yako.

Mafuta kwa ajili ya matumizi yako

Jitahidi utumie mafuta kama ya mizeituni au alizeti katika kuandaa mlo wako