Vyakula vya kiamsha kinywa kwa ajili ya kupunguza uzani

Vyakula vya kiamsha kinywa kwa ajili ya kupunguza uzani

Na MARGARET MAINA

mwmaina@ke.nationmdia.com

Mayai

WATU wengi bado wanaamini kuwa mayai ni mabaya kwa afya yako hasa katika kuongeza lehemu mwilini.

Ukweli ni kwamba ,kila kitu duniani kikitumiwa kwa wingi uliopitiliza huleta madhara fulani.

Mayai yanaweza kusaidia kupunguza uzito kwa sababu yana kiasi kikubwa sana cha Protini inayofanya ujisikie umeshiba kwa muda mrefu sana kwa sababu tumbo huhitaji muda mrefu zaidi kumeng’enya kundi hili la vyakula.

 

Mayai. Picha/ Margaret Maina

Kwa sababu protini hukaa tumboni muda mrefu hukusababisha kuondokana na ile hamu ya kula kula mara kwa mara.

Protini hutengeneza misuli ambayo ndiyo nyenzo kuu katika kuyeyusha mafuta mwilini.

Mtindi

Unaweza kutumia mtindi wenyewe au ukachanganya na vitu vingine ili kubadilisha ladha au kuongeza virutubisho zaidi.

Ili kuongeza protini zaidi kwenye chakula hiki unaweza kuchanganya na karanga au mbegu kama almonds na chia seeds.

Pia unaweza changanya na kipande kidogo cha tunda kama berries au kipande cha ndizi kwa ajili ya kuongeza utamu kwa mbali.

Mtindi na ndizi. Picha/ Margaret Maina

Kikombe kimoja cha maziwa haya wakati wa asubuhi hukufanya ujisikie umeshiba bila kuhitaji kitu zaidi.

Smoothie

Huu ni mchanganyiko wa maziwa na tunda au mboga mboga unaovurugwa kwenye blenda ili kutengeneza kinywaji mfano wa milk shake.

Uzuri mkubwa wa smoothie ni kwamba ni kinywaji kilaini kwa hiyo hata ukinywa kingi tumbo linakuwa jepesi na halichomozi au kujaa gesi.

Changanya matunda yasiyo na sukari sana kama strawberries, zabibu, parachichi, au chochote ukipendacho kwenye maziwa kisha vuruga kwenye blenda.

Smoothie. Picha/ Margaret Maina

Ili kuongeza virutubisho zaidi hasa protini unaweza kuongeza kijiko cha siagi ya karanga, au karanga, almonds, chia seeds, flax seeds na kadhalika

Unaweza pia kutumia kipande kidogo cha tunda lenye sukari kama hauna uzito mkubwa sana, au kijiko cha asali kwa ajili ya kuongeza utamu.

Saladi

Anza mazoea ya kutengeneza kachumbari yenye vitu mbali mbali iliyochanganywa na chakula cha protini kama yai la kuchemsha (salad ya mayai ya kuchemsha) au nyama/samaki/maharage yaliyobaki usiku uliopita.

Uzuri wa saladi kwanza zinashibisha sana kutokana na mboga mboga mbichi pamoja na protini utakayoongeza.

Pia huokoa muda kwasababu ni rahisi kuandaa hata kama haujui kupika unaweza kutengeneza saladi.

You can share this post!

Bayern Munich yadengua Al Ahly na kufuzu kwa fainali ya...

Kang’ata avuliwa madaraka kwa kuanika barua...