Wabunge kukutana kujadili na kupigia kura ripoti kuhusu ufaafu wa Jaji Martha Koome kwa cheo cha Jaji Mkuu

Wabunge kukutana kujadili na kupigia kura ripoti kuhusu ufaafu wa Jaji Martha Koome kwa cheo cha Jaji Mkuu

Na CHARLES WASONGA

WABUNGE wameitwa kwa kikao maalum Jumatano kujadili na kupiga kura ripoti ya kamati ya sheria kuhusu ufaafu wa Jaji Martha Koome kwa wadhifa wa Jaji Mkuu nchini.

Jaji Koome alipigwa msasa Alhamisi wiki alipigwa msasa na Kamati ya Bunge kuhusu Sheria na Masuala ya Kikatiba kubaini ufaafu wake kwa wadhifa huo ambao pia utamtwika hadhi ya kuwa Rais wa Idara ya Mahakama.

Ikiwa uteuzi wake utaidhinishwa na bunge, Jaji huyo mwenye tajriba ya miaka 33 katika ulingo wa sheria atachukua mahala pa David Maraga aliyestaafu mnamo Januari 12, 2021.

Hii ni baada ya Jaji huyo Mkuu wa zamani kutimu umri wa miaka 70, umri ambao kikatiba mtu haruhusiwi kushikilia wadhifa huo.

Bi Koome alipendekezwa na Tume ya Huduma za Mahakama (JSC) kutoka miongoni mwa wagombeaji 10 waliohojiwa kwa cheo hicho mwezi jana.

“Kikao cha kwanza maalum kitaanza Jumatano, Mei 19, 2021 ambapo wabunge wabunge watashughulikia kuidhinishwa kwa Jaji Martha Koome kama Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Kenya na hoja kuhusu msamaha wa ushuru kwa kampuni za asili ya Japan,” Karani wa Bunge la Kitaifa Michael Sialai akasema kwenye taarifa kwa wanahabari Jumanne jioni.

Katika kikao maalum cha pili kitakachoanza saa nane na nusu alasiri, wabunge watajadili ripoti ya Kamati ya Bunge kuhusu Sheria Mbadala kuhusu sheria mbalimbali.

Vile vile, Mswada wa Mifugo, 2021, Mswada wa Unyunyiziaji, 2021 na Mswada wa Marekebisho ya Sheria ya Bima ya Matibabu (NHIF) itajadiliwa.

You can share this post!

Benzema sasa kuchezea Ufaransa kwa mara ya kwanza tangu 2015

KINA CHA FIKRA: Pambana na hali yako ili uiboreshe,...