Habari

Wabunge wanawake wavuruga shughuli za bunge

June 13th, 2019 1 min read

Na CHARLES WASONGA

WABUNGE wote wanawake wamevuruga shughuli za bunge dakika chache kabla ya kikao ambacho kunatarajiwa kusomwa bajeti ya mwaka wa kifedha baada ya wao kuondoka wakilalamikia kupigwa kwa mwenzao Fatuma Gedi.

Gedi ambaye ni mbunge Mwakilishi wa Wanawake wa Kaunti ya Wajir alipigwa makonde na mbunge wa Wajir Mashariki, Rashid Kassim Amin baada ya wawili hao kutofautiana kuhusu suala la bajeti.

Wakiondoka, sauti zimesikika: “Mkamate Rashid), Rashid anafaa kung’atuka, Duale (kiongozi wa wengi katika bunge la kitaifa, Aden Duale) anafaa kung’atuka.

Suala hilo liliibuliwa na Mwakilishi wa Wanawake wa Lamu Mohammed Obbo.

“Mheshimiwa spika, sisi wanawake tuko kwa hatari kuu. Jana (Jumatano) tuliambiwa viti vyetu vitafutiliwa mbali na leo Alhamisi mwenzetu Fatuma Gedi amepigwa vikali,” amesema Obbo.