Wabunge waweka masharti mapya dhidi ya mradi wa ujenzi wa Nairobi Expressway

Wabunge waweka masharti mapya dhidi ya mradi wa ujenzi wa Nairobi Expressway

Na CHARLES WASONGA

WABUNGE wametaka utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa barabara ya moja kwa moja kutoka Uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa Jomo Kenyatta (JKIA) hadi Westlands usianze hadi uchunguzi kuhusu athari zake kijamii na kimazingira (EIA) utakapofanywa.

Kamati ya bunge kuhusu Mazingira na Maliasili pia inaitaka Mamlaka ya Kitaifa ya Barabara Kuu (KeNHA) kuhakikisha vikao vya kukusanya maoni ya umma vinaandaliwa kabla ya kazi hiyo kuanza.

“Hatupingi utekelezaji wa mradi huu, lakini ili kuzui hali ambapo watu fulani watawasilisha kesi kortini kuinga, tunata uchunguzi wa athari zake ufanywe na ripoti iwasilishwe kwa Mamlaka ya Usimamizi wa Mazingira (Nema),” akasema mwenyekiti wa kamati hiyo Kareke Mbiuki kwenye kikao na wanahabari katika majengo ya bunge Jumanne.

Bw Mbiuki amesema kamati yake imetoa sharti hilo baada ya kufahamishwa kwamba mamlaka ya KeHNA imebadili muundo wa awali wa barabara hiyo na kuandaa mpya.

“Kulingana na sheria, ripoti nyingine ya EIA inafaa kuandaliwa na kuwasilishwa kwa Nema. Kaimu Mkurugenzi Mkuu Nema Mamo Boru Mamo ametufahamisha kuwa ripoti ya EIA ya awali sasa haistahili kutumika katika utekelezaji wa mradi huu,” akasema Mbiuki ambaye ni mbunge wa Maara.

Mradi huo utakaogharimu Sh60 bilioni utatekelezwa na kampuni ya China Road and Bridge Company (CRBC) kwa kipindi cha miaka miwili na utalenga kupunguza msongomano wa magari jijini Nairobi.

You can share this post!

Wafanyakazi wa kiwanda cha sukari cha Mumias watimuliwa

Wakazi wa Kiambu wafurahia Sensa ya 2019

adminleo