Wachezaji wa mitaa ya Nakuru wapokea ufadhili kupiga jeki azma yao kusakata soka

Wachezaji wa mitaa ya Nakuru wapokea ufadhili kupiga jeki azma yao kusakata soka

NA RICHARD MAOSI

Timu nyingi za mashinani, zimekuwa zikipitia wakati mgumu wakati wa kusaka ufadhili, labda kutokana na miundo misingi duni mitaani.

Aidha inawezekana soko la kununua wachezaji nchini bado halijaimarika, taifa na wizara ya michezo zikiendelea kutilia shaka uwezo wa wachezaji wa humu nchini.Wiki iliyopita wachezaji wa Nakuru Youth Sports Assoiation(NYSA ) walipokea ufadhili wa jezi, mipira, mabuti na matibabu ya bure kutoka kwa Mediheal Group of Hospitals.

Timu hii ambayo inashiriki ligi ya kaunti kuanzia Olenguruone hadi Naivasha, ilianzishwa mnamo 2011 na mkufunzi Dickson Gitari akiwa na lengo la kuwasaidia vijana mitaani kujitenga na mihadarati na uhuni.

Isitoshe alitazamia kukuza talanta za vijana wa mitaani ambao wengi wao husishia katika lindi la umaskini kwa kutomakinika maishani na kutumia vipaji vyao ipasavyo.

Kikosi cha NYSA ni kwa wachezaji kati ya miaka 5-21, ambapo kwa sasa ni wachezaji 60 ambao hufika uwanjani Afraha kila siku za wiki kufanya mazoezi kwa ajili ya kujiandaa kwa mechi za kujipima nguvu na za ligi.

“Wakati wa likizo tunaweza kupokea hadi wachezaji 200, ambao baadhi yao huja kujifunzi stadi ya kucheza soka ,”alisema.Anasema kuwa kikosi chake kinalenga kufika mbali siku za usoni, akiamini kuwa wachezaji wake watakuja kuwakilisha nchi kwenye michuano ya Hrambe Stars.

Picha/Richard Maosi

Hii ni baada ya kuandikisha msururu wa matokeo mazuri katika ratiba ya jumla ya michuano, kuanzia ile ya kaunti mpaka michuano ya Betway Cup.Alieleza kuwa NYSA ikiwa ni timu ya mtaani imechangia katika akiba ya zana mahiri kwa kuwakuza wachezaji kama Sydney Lokale ambaye amewahi kuchezea timu ya Kariobangi Sharks kwenye ligi ya Kenya Premier League(KPL).

Nahonda wa NYSA Jackson Ongusa aliambia Dimba, atashirikiana na wachezaji wake kuhakikisha wananyanyua taji la msimu huu kutokana na mechi kadhaa zilizosalia

Lakini kwa timu ya Nakuru Youth Sports Association, mambo ni tofauti , hii ndio sababu usimamizi wa Hospital ya Mediheal umeamua kuwafadhili wachezaji wake ambao wengi wao wanatokea familia maskini za mitaa ya Kivumbini, Bondeni, Rhonda, Freehold na Freearea.

Naibu mwenyekiti wa Mediheal Bw Santos Deverey anasema wamekuwa wakifadhili michezo mingi mojawapo ikiwa ni karate, raga na soka.Msimu huu walivutiwa na mafanikio ya NYSA, ndiposa wakafadhili wachezaji kwa jezi, mipira, ushauri nasaha na ukaguzi wa viungo vya mwili bila malipo.

Timu ya Nysa itafaidika na ukaguzi wa matibabu ya bure mbli na kupata nauli na hela za malazi kwa mechi za ugenini ikiwa ni njia mojawapo ya kurudisha shukrani kwenye jamii.

Hatua hii itasaidia kupiga jeki kampeni yao kuwania taji la Betway Cup mwezi ujao katika eneo la Siaya kaunti ya Nyanza,”akasema Santos.Wachezaji wa timu ya Nakuru Youth waonyesha furaha yao baada ya kunufaika na jezi na mipira , katika uwanja wa Afraha.

Baadhi yao wanatokea familia maskini katika mitaa ya mabanda ya Rhonda , Kivumbini na Bondeni.

Picha/Richard Maosi

  • Tags

You can share this post!

Presha Jubilee ilipe deni la Kalembe Ndile kabla ya mazishi...

Obado na kakaye Ruto wakutana kukata miguu Raila eneo la...