Wadudu waharibifu wavamia mashamba ya mahindi Gatundu Kaskazini

Wadudu waharibifu wavamia mashamba ya mahindi Gatundu Kaskazini

Na LAWRENCE ONGARO

WAKAZI wa kijiji cha Kianganga, Mitero, Gatundu Kaskazini wanalalamikia upungufu mahindi katika mashamba yao.

Walidai ya kwamba viwavijeshi wamevamia mahindi kwenye mashamba yao na kusababisha upungufu wa mahindi.

Bernard Chege, ambaye ni mkazi wa kijiji hicho, anasema ni muda wa miaka mitano ambapo wamevuna mahindi kiwango cha chini mno.

“Tunaiomba serikali ifanye juhudi kuona ya kwamba inatuma maafisa wa kilimo vijijini ili kuhamasisha wakulima jinsi ya kukabiliana na wadudu hao,” alieleza Bw Chege na kuongeza kuwa kwa sasa hawajui la kufanya.

Alizidi kueleza kuwa hata mvua inayoendelea kuonyesha imeharibu mazao mengi katika eneo hilo.

Alieleza kuwa jambo muhimu wanalohitaji kutoka kwa serikali ni mbegu za mahindi ili waweze kupanda.

Naye Bi Monica Wanyoike alisema licha ya kufanya bidii na kupanda mahindi kwa wingi amekosa kupata mavuno ya kuridhisha.

“Sisi kama wakulima wa kijiji hiki tumetuma ujumbe kwa serikali kuona ya kwamba maafisa wa kilimo wanakuja mashinani ili kujionea hasara iliyoko kwenye mashamba yetu,” alifafanua Bi Wanyoike.

Bw Bernard Karanja ambaye amekosa mavuno ya kuridhisha ameamua kufuga kuku.

Lakini bado analalamika kwamba kuku wake wanaibwa usiku kumaanisha ni pigo kwa juhudi zake za kilimo na ufugaji wa kuku.

“Hata tunataka machifu wetu watusaidie kuimarisha usalama. Siku hizi maisha yetu ni kama ya paka na panya ya kuviziana kwani hakuna hata usalama wa kutosha,” alifafanua Bw Karanja.

You can share this post!

EPL: Man-City watuma onyo kali kwa washindani wakuu ligini...

BAHARI YA MAPENZI: Ndoa ya njoo tuishi au ya kanisani?

T L