Wafalme Ogier na Loeb kunogesha Safari Rally iliyoshuhudia idadi ya washiriki ikipungua sana

Wafalme Ogier na Loeb kunogesha Safari Rally iliyoshuhudia idadi ya washiriki ikipungua sana

Na GEOFFREY ANENE

ORODHA ya madereva watakaoshiriki Mbio za Magari Duniani (WRC) duru ya Safari Rally imepungua kutoka 58 mwaka 2021 hadi 34 mwaka 2022.

Bingwa mtetezi Sebastien Ogier, ambaye ameshinda taji la dunia mara nane, pamoja na Mfaransa mwenzake Sebastien Loeb, ambaye ni bingwa mara tisa wa dunia, watanogesha katika duru hiyo ya sita itakayoandaliwa Juni 23-26 katika kaunti za Nairobi na Nakuru (Naivasha).

Shirikisho la Mbio za Magari Duniani (FIA) limetangaza orodha hiyo ambayo pia ina madereva matata Kalle Rovanpera aliyenyakua mataji ya duru za Uswidi, Croatia na Ureno, Mbelgiji Thierry Neuville, Mjapani Takamoto Katsuta, Ott Tanak kutoka Estonia na Elfyn Evans kutoka Wales, miongoni mwa wengine.

Madereva kutoka Finland, Ubelgiji, Japan, Estonia, Uingereza, Ireland, Ufaransa, Uswidi, Ugiriki, Poland, Czech, Amerika, India, Zimbabwe, Italia, Uhispania na Kenya wameingia Safari Rally. Karan Patel, ambaye anaongoza mbio za magari za kitaifa za Kenya (KNRC) msimu huu yupo pamoja na madereva McRae Kimathi, Jeremy Wahome, Hamza Anwar na Maxine Wahome ambao wako katika mradi wa kukuzwa na FIA kuwa nyota wa baadaye.

  • Tags

You can share this post!

IEBC yampa Kalonzo muda wa hadi Jumapili Mei 29 kuwasilisha...

Kingi ni msaliti, viongozi wadai

T L