Habari Mseto

Wafanyakazi wa Doshi wakana kuiba nyaya za mamilioni

November 18th, 2020 1 min read

Na RICHARD MUNGUTI

WAFANYAKAZI wanne wa kampuni ya kutengeneza chuma ya Doshi Group Jumanne walikana kuiba nyaya za kutengeneza stima zenye thamani ya Sh69milioni.

Wanne hao Maxwell Mutunga Wambua, Michael Otieno Ogonjo, Mutunga Kitili na Julius Ondara Hezron walishtakiwa katika mahakama ya Milimani Nairobi.

Walikana mbele ya hakimu mkuu Bi Martha Mutuku kwamba waliiba nyaya hizo kati ya Januaru 2018 na Novemb1 2 2020.

Washtakiwa waliomba korti iwaachilie kwa dhamana. Kiongozi wa mashtaka Bw Anderson Gikunda hakupinga ombi hilo.

Hakimu alisema dhamana ni haki ya kila mshtakiwa na kuamuru kila mmoja alipe dhamana ya pesa tasilimu Sh2milioni ama dhamana ya Sh5milioni na mdhamini mmoja wa kiasi sawa na hicho.

Kesi hiyo itatajwa katika muda wa wiki mbili upande wa mashtaka ueleze ikiwa umewakabidhi washtakiwa nakala za ushahidi kuandaa tetezi zao.