Habari Mseto

Waficha nyuso zao kizimbani wakikana mashtaka ya ulaghai wa shamba

September 19th, 2018 1 min read

Na RICHARD MUNGUTI

WANAWAKE wawili Jumanne walifunika nyuso zao kwa shuka waliposhtakiwa kwa ulaghai wa shamba lenye thamani ya Sh135 milioni miaka minane iliyopita.

Bi Jennifer Muthoni Murigi na Winnie Wanjiru Njeri (pichani) walikanusha mashtaka matatu dhidi yao ya ughushi wa stakabadhi za umiliki wa ardhi.

Walishtakiwa mnamo Septemba 28, 2010 wakiwa na nia ya kuilaghai kampuni ya Homeland Investors Limited walijitengenezea cheti cha mauzo ya shamba nambari LR 20523.

Walidai mkataba huo wa mauzo ulikuwa umetayarishwa na wakili Getrude Matata.

Mahakama ilifahamishwa kuwa wawili hao walikabidhi mkataba huo wa mauzo wamiliki wa kampuni hiyo ya Homeland na kuwatepeli sehemu ya shamba lake lenye thamani ya Sh90 milioni. Shamba hilo liko katika eneo la Mavoko, Kaunti ya Machakos

Walikanusha mashtaka na kuachiliwa kwa dhamana ya Sh2 milioni.

Kesi itasikizwa Oktoba 4, 2018.