Habari Mseto

Wafugaji walalamika maziwa kununuliwa kwa bei ya kutupa

Na BARNABAS BII July 10th, 2024 1 min read

WAKULIMA wanaofuga ng’ombe wa maziwa eneo la Magharibi mwa Kenya wanapata hasara baada ya kampuni za kusindika maziwa kupunguza bei ya maziwa kwa Sh8 kutokana na ukosefu wa soko na vifaa vya kuhifadhia maziwa hayo.

Bei ya lita ya maziwa imeshuka kutoka Sh38 hadi 30, huku wakulima wakilalamikia gharama ya juu ya uzalishaji.

Mwenyekiti wa chama cha Wafugaji Ng’ombe wa Maziwa nchini (KDFF), Bw Stanley Ngombe, jana alisema kampuni za maziwa za kibinafsi zimeonya bei hiyo itashuka zaidi.

“Kampuni za kibinafsi zinatoa bei ya chini ya Sh30 kwa lita kinyume na makubaliano yaliyowekwa na Bodi ya Maziwa nchini na Wizara ya Kilimo ya Sh33,” alisema Bw Ngombe.