Wafugaji walia chagamoto kibao zimezingira biashara ya kuku

Wafugaji walia chagamoto kibao zimezingira biashara ya kuku

NA SAMMY WAWERU

WAFUGAJI wa kuku Kiambu wamelalamikia kuongezeka kwa gharama ya ufugaji.

Chini ya kipindi cha miaka mitatu iliyopita, bei ya chakula cha madukani imekuwa ikiandikisha ongezeko wafugaji wakilia kwamba hatua hiyo inatishia biashara.

“Kila ninapoenda dukani kununua chakula, ninapata bei imeongezwa,” ameteta Minnie Ngugi, mfugaji wa kuku wa mayai eneo la Kabuku, Kiambu.

Bi Minnie Ngugi ni mfugaji wa kuku wa mayai Kiambu. PICHA | SAMMY WAWERU

Licha ya mfumko huo wa gharama, mfugaji huyo analalamikia ubora wa chakula cha madukani kuwa wa chini.

“Ninalazimika kutafuta malighafi na virutubisho kutoka kwa wanaouza kwa bei nafuu, nijiundie lishe,” akaelezea mfugaji huyo.

Lalama zake si tofauti na za Joseph Ndung’u, mfugaji eneo la Kabete.

“Serikali mpya iweke mikakati maalum kuokoa sekta ya kuku. Ipunguze bei ya chakula cha kuku na malighafi. Wafugaji tunaumia sana,” Bw Ndung’u akahimiza.

“Tunaonunua vifaranga kuwalea wawe kuku wa mayai, bei haikamatiki,” akalalamika mfugaji huyo ambaye ni naibu mwenyekiti Kabete Poultry Sacco,

Ndung’u amekuwa katika biashara ya kuku kwa zaidi ya miaka 30, naye Bi Ngugi miaka 10, wote wakisema changamoto wanazopitia kwa sasa zimevuka mipaka.

Walitoa malalamishi yao katika hafla iliyoandaliwa na kampuni ya usambazaji kuku na bidhaa za kuku nchini, Kenchic, Kiambu.

Mazao ya kuku; mayai na nyama, bei ya haijapanda, wafugaji wakikadiria hasara.

Sekta ya kuku imetajwa kama iliyoathirika pakubwa na ongezeko la gharama ya chakula cha mifugo.

Ushuru unaotozwa malisho na malighafi, umechangia mfumko huo wa bei.

Baadhi tayari wamelazimika kuacha biashara hiyo, wakifuga kuku wa kutosheleza mahitaji ya familia zao.

Kenya huagiza nje ya nchi zaidi ya asilimia 70 ya malighafi kutengeneza chakula cha mifugo.

  • Tags

You can share this post!

Maafisa watatu wa zamani wa Tana River washtakiwa mjini...

Kufutwa kazi Kulundu kwakera Azimio

T L