Habari Mseto

Wafungwa 219 watoroka jela

September 21st, 2020 1 min read

Daily Monitor

Zaidi ya wafungwa 200 wametoroka jela la Moroto Kaskazini Mashariki mwa Uganda huku maafisa wa polisi wakianza kuwasaka wafungwa hao.

Wafungwa hao wa jela la Singila wanasemekana kutoa sare zao za rangi majaano na kutoroka wakiwa uchi wa mnyama ili wasitambulike.

Afisa mmoja wa jeshi wa Uganda ameripotiwa kufariki wakati wa makabiliano na wafungwa hao.

Jela hilo limejengwa kwenye mlima Moroto ambao uko mpakani mwa mji. Maafisa wa Uganda walisema kwamba waliwakamata wafungwa watatu tayari.

Maafisa wa usalama ambao hawakutaka kutajwa majina kwasababu hawaruhusiwi kuzungumza na wanahabari walisema kwamba wafungwa hao walikuwa 219.

Walinyakua bunduki kutoka kwa walinzi wa jela na kutorokea Mlima Moroto.