Kimataifa

Wafungwa 3 waliotoroka wauawa

September 14th, 2020 1 min read

Na Daily Monitor

Wafungwa watatu ambao walitoroka kwenye jela la Singila Moroto ,Uganda Jumatano wameuawa huku wengine saba wakikamtwa,  mamlaka ya jela imethibitisha.

Bw Frank Baine, msemaji wa jela hilo alisema kwamba idadi ya wafungwa waliotoroka ni 219 kutoka jela ambalo lina idadi ya wafungwa 620.

Bw Baine alisema kwamba baada ya tukio hilo maafisa wa usalama wakiwemo majeshi walijitolea kuwatafuta usiku mzima uku wakipiga doria Mlima Moroto ambapo walitorokea.

“Kufikia asubuhi ya Alhamisi wafungwa saba wamekamatwa tayari na wengine tatu kuuliwa,” alisema

Alisema timu kutoka jela la Soroti imetumwa kusaidia wenzake wa Singila.

“Maafisa wa usalama wameongezwa ili kusaidia kutafuta watoro hao kabla hawajaingia Kenya mabapo itakuwa vigumu kuwapata,” alisema.

Tafsiri na Faustine Ngila