Habari Mseto

Wafungwa sita waliokuwa wametoka hospitalini wahusika kwenye ajali

June 4th, 2024 1 min read

NA GEORGE ODIWUOR

WAFUNGWA sita na polisi watano wa magereza wamejeruhiwa kufuatia ajali ya barabarani iliyotokea mjini Homa Bay Jumanne alasiri.

Ajali hiyo ilitokea wakati karandinga la polisi wa magereza lilipopoteza mwelekeo na kuanguka huku likilalia upande mmoja.

Wafungwa hao walikuwa wameugua na wakati ajali hiyo ilipotokea, walikuwa wanarejeshwa jela la Rachuonyo kutoka hospitalini.

Waliojeruhiwa wamekimbizwa katika Hospitali ya Rufaa ya Homa Bay kwa matibabu.