Habari Mseto

Wafurahia harusi yao licha ya amri za corona

April 14th, 2020 1 min read

Na Lawrence Ongaro

HARUSI ya kipekee ilifanyika mjini Thika Jumatatu na kuhudhuriwa na watu 15 pekee.

Hii ni kutokana na sheria mpya ya serikali kupendekeza mkusanyiko wa watu wachache kufuatia homa ya corona.

Wapendwa wawili Bw Kenneth Mureithi, na Pauline Waithera, walifika katika kanisa la kianglikana la St Andrew Church mjini Thika, ili kufunga pingu za maisha kwenye harusi hiyo.

Jambo la kushangaza ni kwamba zoezi hilo lilichukua muda wa dakika 30, huku kila mmoja akiweka nafasi mbali na mwenzake.

Kanisa ambalo hujaza zaidi ya watu 1,000, lilikuwa na watu 25 pekee pamoja na waandishi wa habari.