Wageni Pwani waonywa kuwa makini baharini

Wageni Pwani waonywa kuwa makini baharini

Na KNA

WAGENI ambao wananuia kuzuru maeneo ya Pwani wakati wa shamrashamra za kufunga mwaka, wameshauriwa kuwa waangalifu hasa wanapojivinjari baharini.

Kamishna wa Kaunti ya Kwale, Bw Gideon Oyagi, aliwataka wageni wasio na ujuzi wa kuogolea baharini watafute usaidizi kwa wataalamu.

“Tuna wataalamu wa kutosha kutoka serikali ya kitaifa na wale walioajiriwa na hoteli. Tumejitolea kulinda kila mgeni,” alihoji.kwa hivyo wageni watapata usaidizi unapofaa. Tumejitolea kulinda kila mgeni,” akasema.

Alitoa ushauri pia watu wasitembelee bahari nyakati za usiku, akisema visa vingi ambavyo baadhi huhusisha vifo huwa vimetokea usiku.

Alisisitiza serikali imeeka usalama wa kutosha katika kipindi hiki cha sherehe.

You can share this post!

Serikali iharakishe miradi ya Italia – Kingi

Jaji akataa malalamiko kuhusu lugha

T L