Habari Mseto

Wahalifu wawaua maafisa wawili wa polisi Kayole

November 8th, 2019 1 min read

Na VINCENT ACHUKA

MAAFISA wawili wa polisi waliokuwa wanapiga doria wameuawa kwa kupigwa risasi katika hali tatanishi Ijumaa asubuhi, Kayole, Nairobi.

Mamlaka zinasema maafisa hao wawili wa cheo cha konstebo na ambao walikuwa wa kituo cha polisi cha Obama walikuwa wanashika doria eneo la Mwenyenge walipovamiwa na wahalifu na kuuawa karibu na daraja la Saika Kayole.

Uhalifu huo ulitekelezwa saa kumi za asubihi.

“Afisa mmoja wa polisi amepigwa risasi kifuani huku mwingine akimiminiwa risasi kichwani,” polisi imesema.

Maganda matano ya risasi zilizotumika yalipatikana katika eneo hilo.

Wahalifu hao wameibwa bunduki za maafisa na simu zao.