Wahamiaji wazidi kufurika Uingereza

Wahamiaji wazidi kufurika Uingereza

Na MASHIRIKA

WAHAMIAJI zaidi ya 430 jana walimiminika Uingereza kupitia kivuko cha baharini cha English Channel, wakiwa kwenye boti ndogo.

Idadi hiyo ni ya juu zaidi kuwahi kurekodiwa kwa siku moja.Walikuwemo watu 50 waliobebwa kwenye chombo kilichotua eneo la Dungeness katika jimbo la Kent.“Baadhi ya watu waliinua mikono yao hewani kama ishara ya kusherehekea kukamilisha safari hiyo hatari huku wengine wakisaidiwa kutembea hadi kwenye ufuo.

“Baadhi ya waliowasili ni wanawake na watoto, wengine wakiwa wachanga mno wasioweza kutembea,” lilisema gazeti la Evening Standard.Takriban wahamiaji 8,000 wamesafiri Uingereza wakitumia jumla ya maboti 345 kufikia sasa mwaka huu, ikiwemo 241 waliowasili Jumapili.

“Waingereza wamechoshwa na mipaka ya wazi na uhamiaji kiholela huku boti zikiwasili kwa njia haramu kwenye fuo zetu na magenge ya wahalifu,” alisema Waziri wa Usalama wa Ndani Priti Patel.

Bungeni.

Tumechoshwa na watu kuzama katika safari hizi hatari, haramu na za kiholela,” alisema Waziri wa Usalama wa Ndani Priti Patel Bungeni.The Guardian ilieleza kuwa idadi hiyo ya jana ilijiri huku wabunge wakijadili Mswada kuhusu Utaifa na Mipaka uliopachikwa jina la “mswada wa kupiga vita wakimbizi” na wakosoaji bungeni.

“Waingereza wamechoshwa na mipaka ya wazi na uhamiaji usiodhibitiwa…tumechoshwa na vyombo vinavyowasili kwa njia haramu kwenye fuo zetu vikiwa vinaongozwa na magenge ya wahalifu. Tumechoshwa na watu kuzama katika safari hizi hatari, haramu na za kiholela,” alisema Waziri wa Usalama wa Ndani Priti Patel Bungeni.

  • Tags

You can share this post!

Kiongozi wa upinzani TZ azuiliwa usiku wa manane

Machifu walivyopora mabilioni ya Covid