Wahanga wa ghasia za 2007 wafidiwe kabla ya Uhuru kutoka mamlakani

Wahanga wa ghasia za 2007 wafidiwe kabla ya Uhuru kutoka mamlakani

Na CHARLES WASONGA

HUKU Rais Uhuru Kenyatta akikamilisha muhula wake wa mwisho asije akasahau kwamba kuna baadhi ya wahanga wa ghasia za baada uchaguzi mkuu wa 2007 ambao hawajafidiwa mpaka sasa.

Kwa mujibu wa mshirikishi wa Wakimbizi wa Ndani kwa Ndani (IDPs) Kaunti ya Nakuru Bi Lucy Njeri, kati ya wanachama wake 200,000 ni 83, 000 pekee waliopokea fidia ya Sh50,000 kila moja.

Wengine 27,000 ambao majina yao yalirejeshwa katika makao makuu ya iliyokuwa Wizara ya Mipango Maalum wamekuwa wakisubiri malipo yao tangu 2014.Sasa Bi Njeri na wenzake wanamuomba Rais Kenyatta aingilie kati suala hilo kusudi wapate fidia yao kabla ya kuondoka kwake afisini baada ya uchaguzi mkuu ujao.

Mnamo Desemba 2017 wakati wa mazishi ya aliyekuwa Gavana wa Bomet Joyce Laboso, Rais Kenyatta alikariri kuwa serikali yake itawafidia IDPs wote.“Tunaelewa kuwa kuna IDPs wengine ambao hawakuwa wamelipwa fidia. Ningependa kuwahakikishia kuwa tutawalipa kila mmoja wao, wawe Nakuru, Bomet, Nyandar

You can share this post!

Covid: Sakata ya uuzaji wa vyeti yaibuka

Raila kushiriki NDC ya Wiper

T L