Wahubiri 400 wapokea mafunzo maalum

Wahubiri 400 wapokea mafunzo maalum

NA LAWRENCE ONGARO

WAHUBIRI wapatao 400 wa Kiambu na miji mingine walikongamana katika kanisa la Happy Church, Juja, ili kuhamasishwa kuhusu mbinu madhubuti za kueneza neno la Mungu.

Aliyeongoza ni Wayne Dorsett ambaye alifika nchini na ujumbe kutoka Marekani.

Wahubiri hao walitoka maeneo ya Kiambu, Murang’a, Meru, na hata Thika.

Dorsett aliyetoka Alabama, Marekani alitoa ujumbe mmoja wa kuombea Kenya kwa sababu ya uchaguzi mkuu ujao.

Aliwashauri wamuombe Mungu ili kulinda nchi isiwe na machafuko.

Aliyeongoza ni Wayne Dorsett ambaye alifika nchini na ujumbe kutoka Marekani. PICHA | LAWRENCE ONGARO

Mhubiri huyo alitoa maelezo kuhusu mafunzo maalum kwa wachungaji ili waelewe jinsi ya kuendesha mahubiri yao.

“Ni muhimu wachungaji kuwa makini wanapohubiri neno la Mungu na ni vyema kuwa na ushirikiano wa karibu na waumini popote pale,” alifafanua Dorsett.

Askofu mkuu wa kanisa la Glory Outreach Assembly la Juja, Bw David Thagana, alisema kongamano hilo la siku tatu lilikuwa la kufana sana kwa sababu “litatuongeza maarifa mengi jinsi ya kuendesha mahubiri yetu.”

Alisema wakati huu wa uchaguzi wachungaji wamehimizwa kuomba kwa bidii ili kuwe na uchaguzi wa amani.

“Wakati wa masomo hayo pia tulifunzwa jinsi ya kutoa maamuzi mazito kukiwa na farakano au mafarakano katika jamii,” alifafanua Askofu Thagana.

Alisema kikundi hicho ni kikubwa na wamejitolea mhanga kuona ya kwamba waliofundishwa yanazalisha matunda katika makanisa yao.

Alitoa wito kwa viongozi kuendesha kampeni zao kwa amani na iwapo matokeo yatatangazwa wayakubali bila kuzua vurugu.

Askofu Joseph Nene Gikonyo wa kanisa la Evangelical Faith of Churches, alisema wakati huu wa uchaguzi ni muhimu ambapo wananchi wanastahili kuwa makini ili kuwachagua viongozi waadilifu na wenye maono.

“Sisi kama viongozi tutakwenda kwa waumini wetu na kuwapa mahubiri yatakayowafaidi. Tutawapa mwongozo wa kudumisha amani na kupendana,” alisema Askofu Gikonyo.

Alisema mafunzo waliyopata ni muhimu na ni vyema kufuata mwongozo huo.

Naye mhubiri wa kanisa la Glory Outreach Assemblies of God Bi Philis Githaiga, alisema mafunzo waliyopewa na wahubiri kutoka Marekani ni muhimu kwao.

Aliiomba serikali iangalia bei za chakula na petroli kwa sababu zimesababisha mzigo kwa mwananchi.

“Wakati huu tutahubiri amani na tutahakikisha tunawahimiza waumini kuombea nchi ili uchaguzi uwe wa amani,” akasema Bi Githaiga.

  • Tags

You can share this post!

Salah na Son wagawana Kiatu cha Dhahabu baada ya kuibuka...

Hofu Mswada kusukuma raia kwa bidhaa ghushi

T L