Habari Mseto

Wahubiri wapokea msaada wa chakula kutoka kwa mbunge

June 27th, 2020 1 min read

NA ERIC MATARA

Zaidi ya wahubiri 300 wamepokea msaada wa chakula, Barakoa na vifaa vingine vya kujikinga dhidi ya maambukizi ya virusi vya corona kutoka kwa mbunge wa Nakuru Mashariki Samuel Arama.

Bw Arama alisema msaada huo ulikuwa wa kuwasaidia wahubiri hao wakati huu mgumu wa janga la corona ambapo makanisa yalifungwa akisema yalikuwa ndio kitenga uchumi kwao.

“Nilitafuta msaada kutoka kwa marafiki akiwemo Waziri wa Usalama Fred Matiang’i na tukapata msaada wa chakula,” alisema.

Tangu serikali iweke mikakati ya kupambana na virusi vya corona ikiwemo kufunga makanisa na marufuku ya mikutano, wafanyakazi wa makanisa wamehangaika mno.

Katibu wa muungano wa wahubiri Nakuru Magharibi Rev Philip Madoya alisema kwamba janga la corona limewaathiri sana wafanyakazi wa makanisa.

“Imekuwa vigumu sana kwetu kukithi mahitaji katika wakati huu mgumu wa janga la corona kwasababu ni kama corona ilimeza sadalka na fungu la kumi,” alisema Pasta Madoya.

“Kanisa huendeshwa kama kampuni zingine. Kampuni ni watu huifanya iitwe kampuni. Wakati watu hawaendi makanisani mambo yamekuwa magumu,”aliongeza.

Tafsiri: Faustine Ngila