Waibuka wa kwanza Nyeri licha ya kuwa ni zeruzeru

Waibuka wa kwanza Nyeri licha ya kuwa ni zeruzeru

Na IRENE MUGO

WANAFUNZI wawili wa kike zeruzeru kutoka familia moja ni kati ya waliong’aa katika mtihani wa KCSE mwaka jana na mwaka huu, licha ya jamii kuwataja kama waliolaaniwa katika kijiji cha Thogori, Kaunti ya Nyeri.

Mama ya wasichana hao pamoja na ndugu yao, Regina Mwangi alisimulia kuwa jamii ilimgeuka kwa kuwa wote walikuwa zeruzeru.Hata hivyo, alijiliwaza akisema matokeo ambayo wamekuwa wakipata katika mitihani ya kitaifa yamekipa kijiji hicho sifa na kumfariji moyoni.

“Watu walitudharau na kusema tulikuwa wanachama wa kundi la watu wanaomwabudu shetani. Nafurahia sana matokeo ya watoto wangu,” akasema Bi Mwangi.

Katika matokeo yaliyotolewa Jumatatu, mmoja wao, Caroline Mugo aliibuka mwanafunzi bora katika Kaunti ya Nyeri kwa kupata A- ya alama 76 na akawa katika nafasi ya 13 kitaifa.

Bi Mugo aliiga mfano wa dadake Eveline Wambui, ambaye pia aliongoza katika KCSE mnamo 2019, wote wakiwa walisomea katika shule ya upili ya Wasichana ya Mahiga.

Mnamo 2012, mwanawe wa kiume ambaye pia ni zeruzeru alikuwa kati ya wanafunzi waliong’aa baada ya kupata alama ya B+ katika Shule ya Wavulana ya Nkubu. Alijiunga na Chuo kikuu cha Kenyatta.Wasichana hao walikiri kwamba maumbile yao yamekuwa yakiwaletea kejeli.

 

You can share this post!

Waliong’aa KCSE wasimulia madhila waliyopitia

CHARLES WASONGA: Serikali inakosea kuwaongezea raia maskini...