Habari Mseto

Waiguru afunga afisi yake sababu ya corona

November 17th, 2020 1 min read

NAFAUSTINE NGILA

Gavana wa Kaunti ya Kirinyaga Governor Anne Waiguru alifunga afisi za makao makuu ya Kaunti hiyo kwenye mji wa Kutus, huku akisema kwamba Jumatatu maambukizi ya corona yameogezeka eneo hilo na vifo vimeripotiwa.

Maafisa wa afya walifunga afisi hizo kwa muda wa wiki mbili ili kuzuia kusambaa kwa virusi vya corona huku maafisa wote wakiagizwa kufanyia kazi nyumbani.

Kmati ya Kaunti na maafisa wakuu wanaitajika kuweka mikakati kuhakikisha kwa idara zaa maana zinafanya kazi huku wakizingatia maangizo ya Wizara ya afya.

Idara ziliagizwa kufanya mikutano mitandaoni na kutumia njia za kiekroniki kusambaza ujumbe.

Maafisa wote wanapaswa kuwa wana fikiwa kwa njia ya simu hasa wakati wa masaa ya kazi na kujibu jumbe za baruapepe.

Gavana Waiguru aliagiza maafisa wa afya kuakikisha kwambamaafisa wite wamepimwa virusi vya corona kwamba dawa imenyunyuziwa kwa vifaa vilivyoathirika.