Habari Mseto

Waiguru asambazia wasichana sodo

October 3rd, 2020 1 min read

Na George Munene

KAUNTI ya Kirinyaga Ijumaa alizindua mpango wa kusambaza sodo kwa wasichana wa shule za eneo hilo.

Mpango huo unalenga kuwanufaisha vijana hao kwa pakiti 27,000 kwa wasichana 9,000 katika kaunti hiyo.

Gavana Anne Waiguru akiongoza hafla ya kusambaza sodo hizo katika Shule ya Wasichana ya Kiamugumo eneobunge la Gichugu, alisema kuwa inasikitisha baadhi ya wasichana hukosa vipindi vya masomo kwa kukosa taulo za hedhi. Zaidi ya wasichana 500 kutoka shule hiyo walinufaika.

Bi Waiguru alisema kuwa kama gavana mwanamke pekee kutoka Mlima Kenya, jukumu lake kuu ni kuwashauri wasichana wadogo ili watimize ndoto zao hata ikiwa ni kuwa Rais wa nchi.