Kimataifa

Waislamu, Wayahudi wapigania msikiti Jerusalem

August 12th, 2019 1 min read

Na AFP

GHASIA zilizuka Jumapili katika Msikiti wa Al-Aqsa mjini Jerusalem pale sherehe ya kidini ya Wayahudi na Waislamu zilipogongana, kila kundi likitaka kushiriki ibada mahala hapo.

Utata ulianza pale Waislamu walipomiminika kwenye lango la kuingia kwenye msikiti huo baada ya taarifa kuenea kwamba Wayuhudi wangeruhusiwa kushiriki ibada yao ya na wao wazuiwe.

Hapo ndipo waliwarushia polisi mawe na viti, hali iliyojibiwa kwa ufyatuaji wa risasi huku ripoti zikiarifu watu 14 walijeruhiwa na wawili wakakamatwa kwenye patashika hiyo.

Kumekuwepo na makubaliano kati ya Israeli na Wapalestina kuwa pande zote zinaruhusiwa kutekeleza ibada nyakati tofauti msikitini humo.

Lakini tarehe za ibada muhimu kwenye kalenda zao zimekuwa zikigongana kwa muda wa miaka mitatu iliyopita. Sherehe hizo ni Eid al-Adha kwa Waislamu na Tisha B’av ya Wayahudi.