Wajackoyah apata mpiga debe anayemfanana

Wajackoyah apata mpiga debe anayemfanana

NA GEORGE ODIWUOR

MWANAMUME mmoja katika Kaunti ya Homa Bay anayefanana na mwaniaji wa Urais, George Wajackoyah amewavutia watu wengi katika kaunti hiyo kwa kuunga mkono manifesto ya Profesa Wajackoyah kuhalalisha bangi.

Elivis Omollo ambaye uso wake unafanana na wa profesa Wajackoyah anaamini kuwa ndoto yake ya kukuza bangi itatimia ikiwa kiongozi wa chama cha Roots atashinda uchaguzi wa Agosti 9.

Kwa sasa, matumuzi ya bangi ni haramu nchini Kenya.

Bw Omollo pia anaamini kuwa uchumi wa nchi na hata wa mtu binafsi unaweza kuimarika kupitia ukuzaji na uuzaji wa bangi.

Japo Kaunti ya Homa Bay inaaminika kuwa ngome la Kinara wa ODM, Raila Odinga, Bw Omollo amejitolea kumpigia debe Profesa Wajackoyah katika Kaunti hiyo akiwa na matumaini kuwa profesa huyo atapata ushindi.

Kumpigia debe mwaniaji huyo wa urais kumempa Bw Omollo umaarufu katika eneo hilo.

Anatembea kila kona akiwajulisha wakazi wa kaunti hiyo manifesto ya kiongozi wa chama cha Roots.

“Wawaniaji wengine wa urais wanatueleza kuhusu kubadilisha uchumi ila hawatuelezi mbinu watakazotumia,” akasema Bw Omollo.

Mbali na hayo, Bw Omollo pia anaamini kwamba Profesa Wajackoyah atakuwa kiongozi asiye na ubaguzi.

  • Tags

You can share this post!

Tume yatangaza nafasi elfu 14 za kazi ya ualimu

Nambari ya simu ‘ya Ruto’ yamulikwa ICC

T L