Habari Mseto

Wajiri yaagiza wafanyakazi warejee ofisini

September 1st, 2020 1 min read

Bruhan Makong

Kaunti ya Wajir imeagiza wafanyakazi wake warejee kazini baada ya miezi nne ya kukaa  nyumbani. Hii ni baada ya usimamizi  wa kaunti hiyo kuwaagiza wafanyakazi wake wasio wa muhimu sana wafanyie kazi nyumbani kwenye shughuli ya kupunguza kusambaa kwa virusi vya corona.

Tangu virusi vya corona viripotiwe Mwezi  Mechi 13 Wajir imeripoti vusa 38 vya corona.Kitambo virusivya corona vilikuwa mingi lakini sasa vinaonekana kupungua.

Kwenye ujumbe alioutoa  katibu wa kaunti hio Abdullahi Hassan Maalim alisema  kwamba Kurudi kazini kutahakikisha huduma sahihi.

“Notisi hii  inapeanwa ili kuwaita wafanyakazi wa kaunti kuruddi kazini ili waendelee kupeana huduma huku wakizingatia miongozo ya wizara ya afya.

Bw Maalim alisema pia virusi hivyo vya corona vitakaa  sana  kwa hivyo watu wanapaswa kujifunza kuishi navyo.

Wakuu wa Idara wanatakiwa kuhakikisha usafi wa maeneo ya kazi na na kuhakikisha kwamba wameweka vituo vya kuoshea mikono,kviyeyuzi,barakoa huku wafanyyakzi wakirudi kazini,”alisema.

 

Tafsiri na Faustine Ngila