Habari

Wakadiria hasara baada ya moto kuteketeza nyumba nne Likoni

October 22nd, 2019 1 min read

Na MISHI GONGO

WAKAZI wanakadiria hasara baada ya moto kuteketeza nyumba nne katika eneo la Kaunda, Likoni, Kaunti ya Mombasa.

Baadhi wamesikika wakidai kuwa moto huo ulioanza saa kumi na moja alfajiri ulianzishwa kwa makusudi.

Hii ni baada ya dumu la dizeli kupatikana katika eneo la mkasa.

Kamanda wa polisi katika eneo hilo Benjamin Rotich amethibitisha tukio hilo akisema kuwa hakuna aliyejeruhiwa katika mkasa huo.