Wakanusha mashtaka 22 kuhusu ulaghai wa Sh48m za ustawishaji eneobunge la Kasarani
Na RICHARD MUNGUTI
WASHUKIWA wa ulaghai wa Sh48 milioni za ustawishaji wa eneobunge la Kasarani wamekanusha mashtaka 22 na kuomba waachiliwe kwa dhamana.
Aliyekuwa mbunge wa eneo hilo Elizabeth Ongoro anayeshtakuwa pamoja na waliofikishwa kizimbani, mahakama imeambiwa yuko Afrika kusini akipokea matibabu.