Habari Mseto

Nyaya za stima zakatwa ghafla Kariobangi South

March 21st, 2020 1 min read

Na GEOFFREY ANENE

MADAI yameibuka kuwa wafanyakazi kutoka kampuni ya kusambaza umeme ya Kenya Power walionekana wakizunguka mtaani Kariobangi South jijini Nairobi siku ya Ijumaa na kuanza kukatia umeme wakazi ambao bili zao hazijalipwa.

Watu wawili wanaodhaniwa kutoka kampuni hiyo walifika mtaani hapa kuendesha kata stima katka nyumba kadhaa kinyume na agizo la serikali linalotaka watu wapunguze kuhamahama ili kudhibiti maambukizi ya virusi hatari vya corona na pia kuwezesha Wakenya kununua bidhaa wanazohitaji baada ya wengi wao kupoteza kazi ama kutatizika kufika katika sehemu zao za kazi.

Rais Uhuru Kenyatta alitangaza siku chache zilizopita kuwa ili kuzuia uenezaji wa virusi hivyo, watu waruhusiwe kufanyia kazi nyumbani, huku huduma nyingi zikisitishwa ili kupunguza mikusayiko ya watu.

Walioshuhudia kisa cha watu kutoka kampuni ya umeme kuja kukata stima walisema kuwa ‘maafisa’ hao walilenga kupata hongo kutoka kwa watu waliokatiwa stima.

Inasemekana kuwa baadhi ya wakazi walianza kushuku watu hao walipogundua wameanza kushukiwa, walitoka sehemu hiyo kwa haraka.